ALMANUSURA KUFA BAADA YA KUCHEZEA CHA MBWA MWIZI, KISA KUBAKA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI

0 comments


Kijana Said (30) akipatiwa maji baada ya kupewa kichapo kikali kutoka kwa wananchi.
MWANAUME anayedaiwa kuwa ni kinara wa ubakaji jijini hapa, Said (30) mkazi wa Mbauda, amenusurika kifo kwa kipigo kutoka kwa raia wenye hasira baada ya kunaswa akitoka kumbaka denti wa kidato cha pili hadi kupoteza fahamu.
Said anayetajwa kuwa ‘mwenyekiti’ wa kundi linalojihusisha na ubakaji, alishambuliwa na wananchi hao baada ya yeye na wenzake watano kukutwa kwenye nyumba inayodaiwa kuwa ya uhalifu iliyopo Muriet, Bon City jijini hapa wakimfanyia kitendo hicho cha kinyama mwanafunzi huyo mwenye umri wa miaka 14.
Mashuhuda wa tukio hilo, akiwemo Mwenyekiti wa Mtaa, Francis Mbise walieleza kuwa mtuhumiwa huyo akiwa na wenzake hao walimbaka usiku kucha msichana huyo aliyetajwa kwa jina moja la Jack, mkazi wa Kwamorombo baada ya kufanikiwa kumrubuni kwa maneno na kumwingiza kwenye nyumba hiyo.
Baada ya kufanya unyama huo usiku kucha, alfajiri  mtuhumiwa huyo alionekana akitoka ndani ya nyumba hiyo akiwa kifua wazi na kukimbia, ndipo wananchi walipomtilia shaka na kumkimbiza na baada ya kukamatwa, aliulizwa kama ni mwizi akakataa  bali alitoka kufanya mapenzi na msichana.
Mbise alisema kuwa wananchi hao waliongozana naye hadi kwenye nyumba hiyo na kumkuta msichana huyo akiwa amelala hajitambui huku sehemu zake za siri zikitoka damu.
Mwenyekiti huyo alisema walipomuhoji kwa nini alikuwa akikimbia, alisema yeye alihofu kuwa msichana waliyembaka amepoteza maisha baada ya kushtuka usingizini na kumwona hajitambui huku wenzake wakiwa hawapo.
Alisema mtuhumiwa huyo alikiri kuunda kundi la ubakaji lenye watu watano likiongozwa na yeye huku wakigeuza makazi ya mmoja wa wahalifu hao kuwa danguro la ubakaji. Ndipo wananchi hao walipoamua kumshushia kipigo cha nguvu kabla ya polisi kufika na kumuokoa.
Watuhumiwa wengine walifanikiwa kukimbia na kutotambulika, lakini wananchi wa eneo hilo wanaendelea
kuwasaka.

Mtuhumiwa huyo alichukuliwa na polisi wenye silaha ndani ya gari aina ya Land Rover lenye namba ya usajili PT 1177 huku akiwa ametapakaa damu usoni

TASWIRA YA AJALI YA BASI LA BURUDANI

0 comments
Basi la Burudani baada ya ajali leo Wilaya ya Handeni, Tanga.Hospitali ya wilaya ya Korogwe.
Majeruhi wakipatiwa matibabu.

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe, Mrisho Gambo ( kushoto) akiangalia mmoja wa majeruhi akipatiwa matibabu.

Manesi wakiendelea na matibabu kwa majeruhi.

Mmoja wa majeruhi akiwa amelazwa kwenye benchi.

Wananchi wakiwa eneo la Hospitali.

Basi la Burudani leo limepata ajali maeneo ya Kabuku - Korogwe , watu 12 hadi sasa wamefariki na majeruhi zaidi ya 55. Watu 4 wamepelekwa MOI na KCMC. Tuwaombee majeruhi.

KWA HABARI ZAIDI LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK HAPO CHINI!